Habari

LIONEL MESSI ATIMIZA MICHEZO 600 KWA BARCELONA …bado kaachwa mbali na Xavi na Iniesta

on

Wakati Barcelona ikiichapa Sevilla 2-1 kwenye mchezo wa La Liga, Lionel Messi alikuwa anasherehekea kutimiza michezo 600 kwa miamba hiyo ya Hispania.
Messi alicheza mchezo wake wa kwanza Barcelona miaka 13 iliyopita chini ya kocha Frank Rijkaard katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Porto iliyokuwa inanolewa na Jose Mourinho Novemba 2003.
Lionel Messi anazidiwa na wachezaji wawili tu – Xavi Hernández aliyeichezea Barcelona michezo 767 na Andrés Iniesta  mwenye michezo 642.
Mshambuliaji huyo alicheza mchezo wake wa kwanza Barcelona akiwa na umri  mdogo wa miaka 17. Hata hivyo heshima ya mchezaji mdogo zaidi  inakwenda kwa Paulino Alcántara aliyecheza mchezo wake wa kwanza akiwa na miaka 15 mwaka 1912.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *