LIVERPOOL MAMBO SWAAFI! Sadio Mane apona


Sadio Mane amerejea kwenye mazoezi ya Liverpool  baada ya kupona maumivu ya nyama za paja.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal, alikuwa nje ya dimba tangu Oktoba 8  alipoumia wakati akiichezea timu yake ya taifa dhidi ya Cape Verde.

Kocha Jurgen Klopp akamkaribisha nyota huyo kwa bashasha kwenye kambi yao ya Melwood ambapo alishiriki vizuri mazoezi ya pamoja.


No comments