LIVERPOOL YAENDELEZA UBABE KWA MARIBOR … Sevilla 2 - 1 Spartak Moscow


Wiki mbili zilizopita, timu ya Maribor ya Slovenia ilikalishwa na Liverpool 7-0, lakini Jumatano usiku, timu hizo zilipokutana tena kwenye mchezo mwingine wa Ligi ya Mabingwa, Liverpool ikaibuka na ushindi wa 3-0.

Katika mchezo hupo wa kundi E, mabao ya Liverpool yalifungwa na Mohamed Salah dakika ya 49, Emre Can dakika ya 64 na Daniel Sturridge dakika ya 90. James Milner akakosa penalti dakika ya 53.

Sevilla ikaichapa 2 - 1 Spartak Moscow katika mchezo mwingine wa kundi E.

No comments