LUIS FIGO ATAMKA ZIDANE ASIWE NA PAPARA REAL MADRID USAJILI WA DIRISHA DOGO


WAKATI dirisha la usajili wa mwezi Januari likikaribia, staa wa zamani wa Real Madrid, Luis Figo (Pichani juu), amesema kuwa klabu hiyo inayonolewa na Zinedine Zidane haina haja ya ‘kupaparika’ kusajili kwa kuwa “bunduki zake ziko sawa”, akimaanisha kuwa bado kuna kikosi kizuri licha ya kuanza msimu kwa kusuasua.

"Hakuna wachezaji ambao wanaweza kuboresha Real Madrid," alisema gwiji huyo wa Kireno akizungumza na gazeti la Bild.

Staa huyo aliyewahi kushinda tuzo ya Ballon D'Or, alikuwa Galactico wa kwanza kusajiliwa na Florentino Perez akitokea Barcelona miaka kumi iliyopita, lakini anaamini kuwa klabu hiyo ni sehemu tofauti sana kwa sasa.

"Ni tofauti na zama zangu," alisema staa huyo aliyekuwa akishambulia akitokea pembeni. "Kabla, Madrid ilikuwa ikijitosa kwa nyota wakubwa, lakini falsafa imebadilika sasa. Inasajili mastaa, lakini vijana wadogo."

No comments