LUKAKU ATARAJIA KUZOMEWA CHELSEA LAKINI AAHIDI KUWATUNGUA


ROMELU LUKAKU anatarajia kuzomewa na mashabiki wa Chelsea kwenye dimba la Stamford Bridge leo jioni - lakini amesema ana kiu kubwa ya kuitungua timu yake hiyo ya zamani.
Mshambuliaji huyo ambaye aliutosa uhamisho wa kurejea Chelsea na kuchagua kujiunga na Manchester United kwa pauni milioni 75 dirisha la kiangazi, anataka kumaliza ukame wake wa kutofunga kwenye mechi sita zilizopita.
Lukaku mwenye umri wa miaka 24, hajafunga goli kwa zaidi ya mwezi baada ya kuwa na mwanzo mzuri ulioshuhudia akifunga magoli 10 katika michezo yake tisa ya mwanzo kwenye michuano yote.

No comments