LWANDAMINA AHAHA KUSAKA DAWA YA KUPANDISHA MORARI YA WACHEZAJI YANGA SC

KOCHA wa timu ya Yanga, George Lwandamina amesema kwamba analazimika kutafuta dawa mbadala ya kupandisha morari ya wachezaji baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.

Lwandamina amesema kwamba kwa uzoefu wake anafahamu namna ambavyo mechi za kimataifa zilizoko kwenye kalenda ya FIFA zinavyoathiri mwenendo wa klabu kwenye michuano ya Ligi ulimwenguni kote.

“Sikutamani sana mapumziko haya yaje wakati huu kwani najua madhara yake kwa maendeleo ya klabu kwenye michuano ya Ligi,” alisema kocha huyo.

“Kuna wakati wachezaji hupoteza utulivu kwenye klabu baada ya kutoka kwenye majukumu ya kimataifa hivyo nalazimika kuja na mbinu mbadala kukabiliana na changamoto hii,” aliongeza.

“Lakini ni mambo ya kawaida kwenye ulimwengu wa soka kwa sababu ratiba za jinsi hii haziko Afrika tu mpaka klabu za Ulaya hukumbana na ugumu huu.”

Mzambia huyo alisema kwamba pamoja na hayo klabu yake itaendelea na ratiba yake ya mazoezi kama kawaida kwa wachezaji waliobakia kikosini.

Lwandamina alimaliza kwa kusema kuwa bado ana imani kwamba kikosi chake bado kina nafasi kubwa ya kutetea taji pamoja na kupata sare kwenye mchezo dhidi ya Singida United ugenini huku wakiwa wameachwa kwa alama tatu na Simba.


Mtibwa ambao walibeba ubingwa wa Ligi Kuu bara misimu ya mwaka 1999 na 2000, wataendelea kuzikosa huduma za mastaa wao muhimu wakiwemo kipa Shabaan Kado na beki Salum Kanoni.

No comments