MAINA BAND YAWAITA MASHABIKI KING D HOTEL SINZA

WAPENZI wote wa dansi jijini Dar es Salaam na maeeo jirani leo wamealikwa kujitokeza kwa wingi ndani ya King D hotel, Sinza Africa Sana ambako Maina Band watakuwa wakiporomosha rhumba la kukata na shoka kuanzia majira ya saa 12:30 jioni.

Mwaliko huo umetolewa na bosi wa bendi hiyo, Liston Maina ambaye amewahakikishia uhondo wapenzi wao watakaofika kupata raha za kibakurutu alizoziita ni za kiutu uzima zaidi.


Jumamosi na Jumapili tutakuwa Mikocheni karibu na Kwa Mwalimu Julius Nyerere, katika kiwanja cha Masters Club ambapo ni sehemu ya wastaarabu inayotoa pia huduma nzuri ya vinywaji na vyakula,” amesema Maina.

No comments