MAMA KANUMBA: LULU ANGEFUNGWA MIAKA 10 AU MITANO INGEKUWA NAFUU


Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba amesema, Elizabeth Michael “Lulu” amefungwa miaka michache kama mtu aliyeiba kuku.

Lulu amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kumuua Kanumba bila kukusudia.

Akiongea na kipindi cha Shilawadu cha Clouds TV, mama Kanumba amesema kama Lulu angefungwa miaka mitano au kumi ingekuwa nafuu.

“Nashukuru kuwa haki imetendeka ingawa kafungwa miaka miwili kama mwizi wa kuku,” alisema Mama Kanumba.

No comments