MAN CITY, LIVERPOOL VITANI KUWANIA SAINI YA BEKI VIRGIL VAN DIJK WA UHOLANZI

KLABU za Manchester City na Liverpool zinapigana vikumbo kuwania saini ya beki wa Uholanzi, Virgil van Dijk ambaye Mourinho alimkosa katika dirisha kubwa la usajili lililopita.

Wakati huohuo kocha Pep Guardiola anaendelea na mpango wake wa kuwania saini ya kiungo wa Schalke, Leon Goretzka ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.


Pep ambaye kikosi chake kinaongoza msimamo wa Ligi kwa alama nane, anataka kukitia makali zaidi kikosi hicho.

No comments