MAN CITY YAFUTA MPANGO WA KUMSAJILI SANCHEZ DIRISHA LA JANUARI

MPANGO wa mshambuliaji wa timu ya Arsenal, Alexis Sanchez raia wa Chile kutua katika kikosi cha Manchester City mwezi Januari umekwama.

Klabu ya Manchester City imefuta mpango wa kumsajili staa huyo mwezi Januari bali inataka kumbeba bure mwishoni mwa msimu.


Manchester City wanakwepa gharama ya uhamisho mwezi Januari hivyo wanaona kheri wasubiri mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu ili wamnase bure.

No comments