MANCHESTER CITY HUU NI MWAKA WAO, BAHATI IPO MIKONONI MWAO …Raheem Sterling aleta kiwewe cha furaha


Manchester City imeifunga Southampton 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England ambao umedhihirisha kuwa licha ya kiwango chao bora, lakini Manchester City pia wanabebwa na bahati.

Kevin de Bruyne aliifungia City bao la kwanza dakika ya 66 ambalo lilidumu hadi dakika ya 75 pale Oriol Romeu alipoisawazishia Southampton.

Ikaonekana dhahiri City wanaelekea kuambulia sare kwenye uwanja wao wa Etihad, lakni mambo yakawa kinyume pale  zilipoongezwa dakika tano kufidia muda wa majeruhi.

Dakika tano zilioongezwa nazo zikaondoka, lakini wakati inangia dakika ya 96, Raheem Sterling akaifungia City bao la ushindi baada ya kugongeana vizuri na Kevin de Bruyne. Uwanja wa Etihad ukalipuka kwa furaha, kocha Pep Guardiola akakumbwa na ‘wazimu’ wa kushangilia kwa furaha kubwa.
  

No comments