MANCHESTER CITY YAICHINJA ARSENAL …Aguero, Jesus kama kawaida yao


Nani ataizima kasi ya Manchester City? Hili ndilo swali kubwa sasa baada ya vinara hao wa Ligi Kuu ya England kuwatungua Arsenal 3-1 kwenye uwanja wa Etihad.

City ilitawala sehemu kubwa ya mchezo, ikitandaza soka la kuonana pamoja na mashambulizi mengi ambayo yangeweza kuangusha karamu kubwa ya magoli iwapo yangetumiwa vizuri.

Dakika ya 19 City wakaandika bao la kwanza kupitia kwa Kevin de Bruyne, goli ambalo lililodumu hadi mapumziko.

Dakika ya 50 City wakapata bao la pili kupitia mkwaju wa penalti wa Sergio Aguero kabla Alexandre Lacazette aliyetokea benchi hajaifungia Arsenal bao pekee dakika ya 65.

Gabriel Jesus aliyeingia kuchukua nafasi ya Aguero, akahitimisha kitabu cha magoli kwa kuifungia City bao la tatu dakika ya 74.

Manchester City (4-3-3): Ederson 6, Walker 6.5, Stones 7.5, Otamendi 7, Delph 6.5, De Bruyne 8, Fernandinho 7, Silva 7.5, Sterling 6.5 (Gundogan 78, 6), Aguero 6.5 (Gabriel Jesus 62, 7), Sane 7 (Bernardo Silva 87). 

Arsenal (4-3-3): Cech 6, Bellerin 6, Koscielny 6.5, Monreal 6, Kolasinac 5, Xhaka 6 (Wilshere 78, 6), Coquelin 5.5 (Lacazette 56, 7), Ramsey 6.5, Ozil 5, Iwobi 6 (Giroud 78, 6), Sanchez 6.5. 

No comments