MANCHESTER UNITED YAIFUMUA WATFORD 4-2 LINGARD AKIFUNGA GOLI LA ‘KICHAWI’


Manchester United imevuna ushindi wa bao 4-2 dhidi ya timu ya Watford kwenye uwanja wa Vicarage Road huku mshambuliaji Jesse Lingard akiiteka ‘show’ dakika za ukingoni.

United ilikuwa mbele 3-0 hadi mapumziko kupitia kwa Ashley Young aliyefunga mara mbili na Anthony Martial.

Kipindi cha pili wenyeji wakacharuka na kupunguza bao moja baada ya lingine kupitia kwa Troy Deeney aliyefunga kwa penalti dakika ya 77 na Abdoulaye Doucoure dakika sita kabla ya mpira kumalizika.

Wakati harufu ya sare ikianza kunukia katika mchezo huo wa Premier League, ndipo ukaja wasaa wa  Jesse Lingard kufanya vitu adimu.


Dakika ya 87 mshabuliaji huyo akapokea mpira katikati ya uwanja na kuanza kuchanja mbuga huku akiwalamba chenga mabeki wa Watford mmoja baada ya mwingine kabla kuukwamisha mpira wavuni.

The French international made no mistake when played through by Romelu Lukaku in the 32nd minute on Tuesday night
Martial akiifungia United bao la tatu
Ashley Young celebrates scoring his second of the night to give the visitors a comfortable cushion in the first-half
Ashley Young akishangilia baada ya kuifungia United bao la pili

No comments