MANCHESTER UNITED YAREJEA KWENYE MAKALI YAKE YAICHAPA NEWCASTLE 4-1 …Pogba aleta raha, Ibra naye arejea, Lukuka amaliza gundu
Manchester United imerejea kwenye makali yake baada ya kuiangushia kisago kizito Newcastle cha bao 4-1 kwenye dimba la Old Trafford katika mchezo mkali wa Premier League.

Hata hivyo ni Newcastle ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuiduwaza Manchester United baada ya Dwight Gayle kufunga katika dakika ya 16.

Anthony Martial akaisawazishia United dakika ya 37 baada ya kupokea pasi safi ya kiungo Paul Pogba ambaye ndiyo kwanza amerejea uwanjani baada ya kupona.

Wakati kila mtu akiamini kuwa timu hizo zitakwenda mapumziko zikiwa sare, Chris Smalling akaifungia Manchester United bao la pili dakika ya 45 kufuatia krosi safi ya Ashley Young. Paul Pogba akapiga la tatu dakika ya 54.

Kunako dakika ya 70, Romelu Lukaku akafuta gundu lake la mechi saba bila bao lolote, kwa kuifungia Manchester United bao 4.

Wakati Pogba aliyecheza kwa dakika 69 akitakata vilivyo kwa pasi zake za vipimo, United ikapata furaha nyingine pale mashambuliaji mkongwe Zlatan Ibrahimovic alipoingia uwanjani dakika ya 77, hii ikiwa ni baada ya kuwa nje ya dimba kwa miezi nane kufuatia maumivu ya goti.

Kwa matokeo hayo, Manchester United inaweka rekodi mpya Old Trafford kwa kucheza mechi 39 bila kupoteza mchezo kwenye uwanja wao huo wa nyumbani.

MANCHESTER UNITED (4-1-4-1): De Gea 6; Valencia 6.5, Smalling 7, Lindelof 5.5, Young 7; Matic 6.5; Rashford 6, Mata 7.5 (Herrera 83), Pogba 8 (Fellaini 70 6), Martial 7 (Ibrahimovic 77 6); Lukaku 7 77)

NEWCASTLE (4-4-2): Elliot 6; Yedlin 6.5, Clark 6.5, Lejeune 6.5, Manquillo 6; Murphy 6, Shelvey 7, Hayden 6.5, Ritchie 6.5 (Aarons 66 6); Joselu 5.5 (Mitrovic 71 5.5), Gayle 6.5 (Diame 77 6)


No comments