MARK BAND ALHAMISI HII SLIPWAY, JUMAMOSI NA JUMAPILI CAPE TOWN

ALHAMISI hii The Mark International Band iliyo chini ya Professor Rashid Pembe inatarajiwa kuliamsha dude kama ilivyo ada yake, ambapo itamwaga burudani ya kukata na shoka ndani ya Slipway Hotel, kuanzia majira ya saa 1:00 jioni na kuendelea hadi baadae.

Jumamosi na Jumapili bendi hiyo itakuwa ndani ya Cape Town Fish Market, Msasani jijini Dar es Salaam kuanzia milango ya saa 12 jioni hadi saa 5:00 usiku ambapo muziki mnene kutoka mataifa yote utarindimishwa na wakali hao.


Wanamuziki wanaounda Mark Band ni pamoja na waimbaji Balusi Kitembo, Deus Mgunda na Havile, huku kwenye ala kukiwa na Professor Rashid Pembe (Sax), Faljala Mbutu (Gitaa la Besi), Saad Majivu (Drums), Omari Pembe (Kinanda), Alex Sinkamba (Gitaa la Solo).

No comments