MBEYA CITY "NYANYA" YAIKAMIA SINGIDA UNITED KUFUTA AIBU YA YANGA

TIMU ya Mbeya City imepania kufuta aibu ya mabao 5-0 waliyoipata baada ya kufungwa na Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Jumapili ya wiki iliyopita katika uwanja wa uhuru.

Klabu hiyo imepania kulipa kisasi hicho kwa kuifunga timu ya Singida United katika mchezo utakaopigwa Novemba 25 katika uwanja wa Jamhuri.

Afisa Habari wa Mbeya City, Shaha Mjanja amesema kuwa wamejichimbia mkoani Morogoro wakijiandaa na mchezo huo ambao ameutaja kuwa ni wa kisasi ili kurejesha hali ya ushindi kwa wachezaji.

“Tupo hapa Morogoro tangu juzi na kocha alikuwa akitazama ni wapi tulikosea kwenye mechi dhidi ya Yanga, nikuhakikishie tu kuwa kikosi kiko salama na tuna kila sababu ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wetu ujao,” alisema Afisa Habari huyo.

“Tumeamua kukaa hapa kwa sababu mazingira ni tulivu lakini pia sio mbali na uwanja uliopo, wachezaji wana hali nzuri na wamesahau yaliyopita kwani nafasi ya kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza bado ipo.”


Huu utakuwa mchezo wa pili ugenini kwa Mbeya City baada ya hapo awali kucheza na Yanga jijini Dar es Salaam.

No comments