MBWANA SAMATTA AWASHUKURU WATANZANIA KWA DUA LILILOFANIKISHA UPASUAJI WAKWE WA GOTI

NAHODHA wa kikosi cha Taifa Stars, Mbwana Samatta ameshukuru dua za Watanzania baada ya upasuaji wake wa goti kufanyika salama ambapo atakuwa nje ya uwanja mpaka mwezi Januari.

Staa huyo wa KRC Genk ya nchini Ubelgiji aliumia goti November 4, 2017 wakati  wakicheza mchezo wa Ligi dhidi ya timu ya Lokeren ambao ulimalizika kwa suluhu.

Ni taarifa njema kwa Watanzania wote hususan wadau wa soka kwamba nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta upasuaji wake wa goti umefanyika na kumalizika salama.

Samatta alitumia ukurasa wake wa Instagram kuthibitisha kufanyika salama kwa upasuaji wake sambamba na kushukuru dua za Watanzania ambao walikuwa nyuma yake.

“Napenda kuwajulisha kuwa, upasuaji wangu umeenda vizuri. Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, timu ya madaktari pamoja na mashabiki wangu.”

“Nimepokea meseji nyingi kutoka sehemu tofauti duniani na napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana kwa meseji na Dua zenu hasaWatanzania wenzangu.”


Baada ya kukamilika upasuaji wa Samatta ameshauriwa na madaktari kukaa nje ya uwanja kwa kwa takribani wiki sita ili aweze kupona kabisa.

No comments