MJENGONI CLASSIC BAND KUISIMAMISHA ARUSHA LEO USIKU …Saida Karoli ‘live’ na bendi yake


MJI wa Arusha na vitongoji vyake unatarajia kusimama hapo leo usiku wakati wafalme wa Jiji, Mjengoni Classic Band watakapokuwa wakishereherekea mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwao na kuzundua albamu yao iitwayo “Afadhali”.

Hili ni onyesho kubwa ambalo pia linamshirikisha malkia wa Afro Pop, Saida Karoli ambaye naye atapanda jukwaani na bendi yake ya kuwachezesha wakazi wa Arusha.

Huku itakuwa Saida na Orugamba kule ni Mjengoni Classsic na Tunatosheka na Afadhali. Ni katika ukumbi wa Mjengoni uliopo Olasity, jijini Arusha ambapo kiingilio kitakuwa sh 10,000 tu.

Digitalee Mukongya ‘Tiger’ atakuwa akiongoza mashambulizi sambamba na, Donaa Zinganguvu ‘Chokoraa’ ambaye alitamba na bendi ya Beta Musica sambamba na Sauti ya Radi ambaye alianza kufahamika na Diamond Musica kabla ya kujiunga na Mashujaa.

Lakini pia yupo Sele Mumba  aliyepitia bendi kadhaa zikiwemo Double M Sound na Twanga Pepeta.

Yupo pia Mardosher ambaye ni mwimbaji na Kiongozi wa bendi, Khalid Mumba (rythim), Peter John (Drums), Saleh Tumba, Baraka Machine (kinanda),  wakati waimbaji ni Jonico Peter, Hamza Floris,  Daniel ‘Star’ Eliya, Princes Jean na George Luwela ‘Maria Rosa’.

Baadhi ya nyimbo zinazounda albam mpya ya “Afadhali”  ambayo itazinduliwa sambamba na DVD, ni “Kimbunga” huu ni utunzi wake Donaa, “Jenny” ikiwa  ni kazi yake Jures, “Ni Wabaya” utunzi wake Jonico.

Akizungumzia uzinduzi huo, Digitalee amesema kila kitu kiko sawa kuanzia sound, stage, mavazi namna ya ukaaji pamoja na  wanamuziki wake.

“Tuko imara kabisa, kila kitu kinakwenda vizuri, wanamuziki wako kwenye ari ya juu sana kwa ajili ya onyesho hili…tunataka kuweka heshima ya muziki wa dansi, tunataka kuweka historia na kurudisha heshima ya mikoani.

Kwa upande wake, malkia wa bendi ya hiyo Princess Jean amesema anataka kubadilisha mtazamo wa mashakibi wa muziki wa dansi kuwa muziki upo Dar es Salaam yake.

Naye Repa, mwimbaji, mpiga gitaa na Drums na mtunzi, Donaa Zinganguvu amesema yeye anataka kutumia uzoefu alioupata kwenye bendi za Achigo, Akudo na Beta Musica kuweka ladha nyingine Arusha.

“Mimi Arusha ni mwenyeji, kambi yetu ya kwanza na Beta Musica kabla ya uzinduzi tulikaa hapa mwezi mzima…naijua Arusha, najua wakazi wake wanataka nini, tufanya kitu kikubwa sana,” amesema.

Naye Yanick  Noah maarufu kama Sauti ya Radi amesema leo anakuja na vitu vipya kabisa kuanzia staili ya uingiaji mpangilio wa shoo hata mavazi.

“Hatutaki kuongea mengi lakini hili litakuwa somo kwa mabendi mengine, wajipange nini cha kufanya kwenye uzinduzi wao …rap mpya ambazo ziko kwenye albamu yetu ya “Afadhali” zitasikika hapo, hapo baadae”.

Imeandikwa na Petter David Mwendapole
Mwimbaji Dan Star wa Mjengoni Classic Band
Mwimbaji George Luwena 'Maria Rosa'
Mpiga Drums Peter Machine


No comments