MKE WA RASHID PEMBE KUFANYIWA UPASUAJI JUMATANO

MKE wa mpulizaji mkongwe wa Saxaphone “Domo la Bata”, Rashid Pembe “Profesor”, Fatuma K Msese anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa tumbo kwa ajili ya kutolewa uvimbe unaomsumbua kwa muda mrefu sasa.

Fatuma Msese atafanyiwa upasuaji huo siku ya Jumatano katika hospitali ya Kairuki iliyopo mikocheni, jijini Dar es Salaam alikolazwa tangu jana.

Pembe (pichani), aliyeongea na Saluti5 muda mfupi uliopita, amesema kuwa kinachoendelea sasa ni zoezi la kuwekewa damu kwa mgonjwa huyo ambapo baada ya hapo, kwa mujibu wa madaktari, Jumatano hii ndipo atafanyiwa upasuaji huo.


“Wanaohitaji kumuona mgonjwa wanaweza kufika hospitali ya Kailuki ghorofa ya kwanza, wadi namba 2, chumba namba 5 alikolazwa akisubiri upasuaji huo,” amesema Pembe aliyewahi kutikisa na bendi za Polisi Jazz na Vijana Pambamoto.

No comments