MO DEWJI AVUNJA UKIMYA KUHUSU MASTRAIKA WAZEMBE SIMBA SC

IMEELEZWA kwamba mfadhili wa Simba, Mohammed Dewji “MO” amevunja ukimya ndani ya kambi ya timu hiyo akisema tatizo sio kocha wao, Joseph Omog bali ni kutokujituma kwa mastaa wengi, hasa wale wa kigeni.

Mmoja wa mabosi wa Simba ambaye alikerwa na kiwango cha Simba, amesema katika mazungumzo yake na MO amechukizwa na uwezo mdogo wa wachezaji wao.

Bosi huyo amesema MO ameitaka Simba isisite kuwatimua mastaa wanaoonekana mzigo katika kikosi chao, kauli ambayo inazidi kuwajaza presha mapro wa Simba.

Kauli hiyo haitakuwa taarifa njema kwa mastaa hao wakiwemo wengi wa kigeni kutokana na kutoonyesha uwezo wao ambao hadi sasa hawajafanikiwa kusababisha bao lolote katika kikosi hicho achiliambali kufunga hata bao la kuotea.

“Kiukweli tajiri (MO), hana furaha na kiwango cha timu na yeye hasemi kama kocha ni tatizo kama wenzetu wengine, yeye analia na wachezaji wote,” alisema bosi huyo.


“Amesema hakubaliani na uwezo wa wachezaji wetu, hasa hawa wa kigeni, anasema ukiondoa Okwi wengine ni kama wanawasindikiza wenzao.”

No comments