MORATA AMNYAMAZISHA MOURINHO …Chelsea 1, Manchester United 0


Manchester United imejiweka kwenye mazingira magumu ya kusaka taji la Premier League baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Chelsea.

Bao pekee la Chelsea katika mchezo huo uliochezwa Stamford Bridge, lilifungwa kwa kichwa na mshambuliaji Alvaro Morata kunako dakika ya 55.

United ilicheza soka bovu kwa muda wote wa mchezo ukiondoa dakika 10 za mwisho ambazo ndizo zilizorejesha uhai wa kikosi cha Jose Mourinho.

Kwa ushindi huo Chelsea imefikisha pointi 22, pointi moja nyuma ya Manchester United na Tottenham zenye pointi 23.

Baada ya mchezo, kocha wa Chelsea Antonio Conte alishikwa na kiwewe cha furaha na hakuwa na muda wa kwenda kumpa mkono mpinzani wake, Jose Mourinho.

No comments