MOURINHO AIAMBIA REAL MADRID: "GARETH BALE WENU KIMEO, SIMSAJILI"

KOCHA jeuri wa timu ya Manchester United, Jose Mourinho ameiambia Real Madrid kwamba hatamsajili mshambuliaji wake, Gareth Bale mwenye miaka 28.

Staa huyo amekalia kuti kavu kwenye kikosi hicho cha Real Madrid na suala la majeruhi ya mara kwa mara limezidi kuwa pigo kwake.


Mourinho anafahamu kuwa Madrid wanataka kutengeneza fedha nyingi kwa wachezaji ambao afya zao hazieleweki.

No comments