MOURINHO AMVUMBUA MRITHI WA MICHAEL CARRICK

Achana na ushindi wa 2-0 dhidi ya Benfica kwenye mchezo wa Champions League uliochezwa Jumanne usiku, kinda Scott McTominay ndiye aliyezua gumzo zaidi.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Old Trafford McTominay mwenye umri wa miaka 20, alicheza vema sehemu ya kiungo.
Ukiwa ni mchezo wake wa kwanza kuanza katika Champions League, McTominay akasimama imara huku akishirikiana na  kiungo mkabaji Nemanja Matic.
Kwa kiwango alichokionyesha kinda huyo, mashabiki wa Manchester United wanaamini klabu imempata mbadala sahihi wa kiungo mkongwe Michael Carrick.
Akiongea baada ya mchezo huo, McTominay ambaye amekuwa kwenye academy ya Manchester United tangu akiwa na umri wa miaka mitano, akasema: “Ndoto yangu imetimia”.

No comments