MOURINHO ASEMA KWA FELLAINI WACHA TU AONDOKE BURE


KLABU ya Manchester United iko tayari kumruhusu kiungo wake, Marouane Fellaini kuondoka bila malipo mwishoni mwa msimu huu kuliko kumuuza katika dirisha dogo la Januari.

Mkataba wa Fellaini unaisha mwezi Juni mwakani na United walianza mazungumzo na Mbelgiji huyo kuhusiana na mkataba mpya msimu uliopita, hadi sasa hawajafikia makubaliano.

Mourinho amekuwa akihusudu uchezaji wa kibabe wa kiungo huyo ambaye amekuwa akitokea benchi na kuingia kusaidia ulinzi.

No comments