MOURINHO AWEKA WAZI HABARI ZA ‘BIFU’ LAKE NA ANDER HERRERA

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amefunguka juu uvumi kuwa hana maelewano na kiungo Ander Herrera.
Baada ya kipigo cha 2-1 kutoka kwa Huddersfield  mwezi uliopita, Ander Herrera akatoa maoni kuwa wachezaji hawakuwa na mtazamo hasi na mchezo huo na kwamba ari ilikuwa chini.
Mourinho akasema ni vema wachezaji wakaitisha mkutano wa waandishi wa habari na kuwaomba radhi mashabiki wa Manchester United juu ya hali hiyo.
Maoni hayo yakatafsiriwa vibaya na vyombo vya habari vikiamini kuwa Mourinho hakufurahishwa na maoni ya Herrera.
Lakini Mourinho ameweka wazi kuwa alifurahia maoni ya Herrera. "Nawapenda wachezaji wangu, mnajaribu kupika habari, sina tatizo lolote na Herrera." alisema Mourinho.

No comments