MPAMBANO (EL CLASICO) WA MUUMIN, NYOSHI, CHOCKY KURUDIWA IJUMAA IJAYO TABATA SEGE


Lile pambano kubwa la magwiji wa dansi (El Clasico) kati ya Mwinjuma Muumin, Nyoshi el Sadaat na Ally Chocky, unarudiwa tena Ijumaa hii jijini Dar es Salaam.

Pambano la kwanza la magwiji hao lilifanyika Escape One miezi kadhaa iliyopita lakini likakatishwa na mvua huku Muumin akiwa gwiji pekee aliyebahatika kutumbuiza kabla ya mvua kuharibu onyesho.

El Clasico ya safari hii itafanyika Tabata Segerea katika ukumbi wa Rufita Park ambao ulizinduliwa hivi karibuni baada ya ukarabati mkubwa.

Magwiji wote watatu wameithibitishia Saluti5 kuwa kila kitu kuhusu mpambano huo kimekamilika.

Wakati Muumin atakuwa na bendi yake ya Double M Plus, Chocky na Nyoshi watakuwa na vijana wao watiifu ambao wapo tayari popote pale wanapohitajika. Kwa kifupi kila gwiji atakuwa ‘live’ na bendi iliyokamilika kila eneo.

No comments