MSAFIRI DIOUF AONGEZA NGUVU TWANGA PEPETA …awa ‘stage master’ wa bendi


Rapa na mwimbaji maarufu, Msafiri Diouf amerejea kuitumikia bendi yake ya zamani Twanga Pepeta na atafanya hivyo hadi mwisho wa likizo yake.

Msafiri Diouf ambaye anafanya kazi ya muziki huko Uingereza, awali likizo yake ilikuwa iwe ya miezi mitatu, lakini sasa habari kutoka ndani ya Twanga Pepeta zinasema msanii huyo ataendelea kuwepo nchini hadi mwanzoni mwa mwaka ujao …pengine Januari au Februari au labda mwezi Machi.

Diouf alirejea Bongo mwanzoni kabisa mwa mwezi Septemba na miongoni mwa mipango yake mikubwa, ilikuwa ni kurekodi nyimbo zake binafsi nje ya miondoko ya dansi na tayari ngoma yake moja “The Bridges” ya sweet reggae, ipo hewani.


Meneja wa Twanga Pepeta, Martin Sospeter ameiambia Saluti5 kuwa Diouf kwa sasa ni sehemu ya wasanii wa Twanga Pepeta na amekabidhiwa cheo cha mkuu wa jukwaa (stage master).

Uwepo wa Diouf ndani ya Twanga Pepeta, umeongeza nguvu kubwa ndani ya bendi hiyo ambapo amekuwa 'akiyateka' maonyesho karibu yote aliyoshiriki kwa siku za karibuni.

No comments