MSAKO WA KIPA MPYA REAL MADRID WAMKATISHA TAMAA KEYLOR NAVAS ...Liverpool watia mkono


LIVERPOOL imeripotiwa kuwa na nia ya kumsajili kipa wa kimataifa wa Costa Rica anayeichezea Real Madrid, Keylor Navas mwisho wa msimu na kocha Jurgen Klopp anadaiwa tayari ameanza kufanya mawasiliano juu ya mpango huo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Diario Gol, Navas ameelezwa kutokuwa na furaha katikati ya tetesi kwamba Rais wa Madrid, Florentino Perez yuko sokoni kusaka kipa mpya.

Msako wa kipa mpya ambao umekuwa ukifanywa na Real Madrid katika kila dirisha la usajili, umemfanya Navas aamini kuwa yeye ni suluhisho la muda mfupi ndani ya klabu hiyo.

Kwa mismu kadhaa, Real Madrid imejaribu bila mafanikio kumsajili kipa wa Manchester United David De Gea.

No comments