MSONDO NGOMA KAMA KAWA BULYAGA TEMEKE LEO

MSONDO Ngoma Music Band leo Jumapili kama ilivyo kawaida yake itamalizia uhondo wa burudani kwa wiki hii ndani ya kiwanja cha kujidai cha Bulyaga Temeke, jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 2:00 usiku na kuendelea hadi majogoo.

Taarifa kutoka ndani ya Msondo zinasema kuwa bendi hiyo inayokusanya wanamuziki wengi mahiri na wenye uwezo mkubwa imejipanga kikamilifu kusuuza nafsi za mashabiki wao watakaohudhuria shoo ya leo kwa kuwaporomoshea uhondo mzito.


Msondo Ngoma hutumbuiza ndani ya Bulyaga kila Jumapili na kuonekana kufunika kutokana na shoo yao hiyo kuhudhuriwa na mashabiki wengi zaidi.

No comments