MSONDO NGOMA WAANIKA RATIBA YAO YA WIKI

MSONDO Ngoma Music Band wamewakumbusha mashabiki wao kuwa ratiba ya burudani bado haijabadilika kwa upande wa bendi hiyo ambapo leo Jumatano wataanzia Sugar Ray, Temeke Sokota, jijini Dar es Salaam.

Kesho Alhamisi uhondo utahamia Kisuma Mwembe Yanga na Ijumaa Kisuma ya Magomeni Usalama, huku Jumamosi ikiwa ni zamu ya mashabiki wao wa Buza watakapokuwa wakitumbuiza Dar Safari Park, kabla ya Jumapili kuhitimisha ndani ya New Bulyaga Temeke, jijini Dar es Salaam.

Katika shoo za wiki hii Msondo Ngoma inatarajiwa kutambulisha wasanii wao wapya pamoja na vibao ambavyo ni maandalizi ya albamu yao mpya kabisa.

No comments