MSUVA AWASILI BONGO KUONGEZA NGUVU KIKOSINI STARS

WAKATI timu ya Yanga ikiwa dimbani kucheza dhidi ya Singida United,  winga Simon Msuva alikuwa akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwl. Nyerere kuja kujiunga na kambi ya timu ya Taifa Stars inayojiandaa kukabiliana na Benin.

Mshambuliaji huyo ameingia Jumamosi siku ambayo Yanga ilipata sare ya Singida ugenini ambao walikuwa wanauzindua uwanja wao Namfua.

Msuva ndio mfungaji wa mabao yote matatu ya Taifa Stars katika mechi mbili zilizopita, ikishinda 2-0 dhidi ya Botswana Septemba 3 na ikitoa sare ya 1-1 na Malawi October 7, uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Baada ya mechi hizo mfululizo kwenye uwanja wa nyumbani Taifa Stars itatoka mwezi huu kwenda Benin kucheza na wenyeji Novemba 11, mwaka huu na kikosi cha wachezaji 24 ambacho kitasafiri Novemba 9 kwenda Benin tayari kwa mchezo huo.

Kikosi kamili cha Taifa Stars sasa ni makipa; Aishi Manula, Peter Manyika na Ramadhani Kabwili, mabeki Boniphace Maganga, Abdi Banda, Gardiel Michael, Kevin Yondan, Nurdin Chona na Dickson Job.


Viungo ni Himid Mao, Mudathir Yahya, Hamisi Abdallah, Jonas Mkude, Raphael Daudi, Simon Msuva, Shiza Kichuya, Ibrahimu Ajib, Mohammed Issa, Farid Mussa na Abdul Mohammed na washambuliaji Mbwana Samatta, Mbaraka Yussuf, Elias Maguri na Yohanna Nkomola.

No comments