MTOTO WA ALLY CHOCKY NAYE AJITOSA KWENYE MUZIKI


Mtoto wa kiume wa mwanamuziki nyota wa dansi, Ally Chocky, amejitosa kwenye muziki ambapo mara kadhaa amekuwa akionekana kwenye majukwaa mbali mbali likiwemo la Mapacha Watatu Original.

Mwezi uliopita Khalid Chokoraa alimpandisha jukwaani mtoto huyo wa Ally Chocky anayejiita Chocky Junior na kusema bendi yake ya Mapacha Watatu itakuwa ikimtumia kwenye baadhi ya maonyesho yake.

Katika onyesho hilo la Mapacha Watatu lililofanyika Brazil Pub, Tegeta, mtoto huyo wa Chocky aliwavutia wengi kwa uimbaji wake ingawa alionekana kuegemea zaidi muziki wa bongo fleva.
Chocky Junior (kulia) akiwa na Chokoraa kwenye jukwaa la Mapacha Watatu

No comments