MUUMIN ASEMA KUNA KITUO CHA RADIO KINA MBEBA CHRISTIAN BELLA


Mwimbaji na mmiliki wa Double M Plus, Mwinjuma Muumin amesema kuna kituo cha radio kina mbeba Christian Bella kwa maslahi yao binafsi.

Muumin ameyasema hayo katika maongezi yake na kituo cha 98.5 AM FM Radio cha jijini Dar es Salaam ambapo pia alisema muziki wa dansi unapunguzwa makali na vituo vya radio na televisheni.

Mwimbaji huyo alisema: “Muziki wa dansi uko chini kwasababu vituo vya radio vimegeemea kwenye bongo fleva, singeli na taarab.

“Sasa hivi mtu wa dansi ambaye yuko juu ni Christian Bella na hiyo ni kwasababu kuna kituo cha radio kina mbeba kwaajili ya maslahi yao binafisi.

“Bella anabebwa, lakini kiukweli kabisa leo umsimamishe Bella na Muumin halafu uwaambie wapige muziki wa kweli, anaweza akakimbia mtu hapo”.

No comments