MUZIKI WA MOHAMED SALAH SI WA KITOTO, LIVERPOOL IMELAMBA DUME

Kama kuna pesa ilikwenda kihalali basi ni zile walizotoa Liverpool kumnunua Mohamed Salah, nyota wa kimataifa wa Misri ambaye tangu atue Anfield dirisha la kiangazi, amekuwa akiibeba timu mabegani mwake.
Aliigharimu Liverpool pauni milioni 34.5 pale walipomsajili kutoka Roma ya Italia, lakini kwa yale anayoyafanya, ni wazi kuwa Liverpool imelamba dume.
Kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya West Ham, Salah alifunga mara mbili katika ushindi wa bao 4-1, hatua inayomfanya ajikusanyie jumla ya mabao saba akilingana na Sergio Ag├╝ero, Romelu Lukaku na Raheem Sterling, bao moja nyuma ya kinara Harry Kane.
Uwezo wake wa kuwachambua mabeki, utulivu anapoingia kwenye 18 ya lango la adui, umemfanya awe mmoja wa washambuliaji hatari katika Premier League.

No comments