MWINJUMA MUUMIN ANADI "LIVE" VIUNO VYA WANENGUAJI WAKE

MWINJUMA Muumin “Kocha wa Dunia” amewaomba mashabiki wa miondoko ya dansi kujitokeza kwa wingi zaidi kwenye shoo yake ya kila Jumapili ndani ya Mikwambe.

“Double M Plus inajiandaa na safari ndeeefu ya kuwapa watu burudani, hata hivyo tunawakaribisha wote pale Mikwambe tunakotumbuiza kila Jumapili kupata vitu adimu kabisa,” amesema Muumin.


Nguli huyo amesema kuwa watakaofika kwenye shoo hiyo, pamoja na burudani nyingine, watafaidi pia kupata uhondo wa shoo yao kali kutoka kwa wanenguaji wao mahiri na wenye uwezo mkubwa wa kumwaga viuno.

No comments