PAUL INCE ATAJA MAPUNGUFU ALIYOYAGUNDUA KWA MANCHESTER UNITED YA JOSE MOURINHO


Kiungo wa zamani wa Manchester United Paul Ince, amesema kikosi cha Jose Mourinho kinakosa mchezaji kiongozi uwanjani.

United iko nyuma ya vinara wa Ligi Kuu ya England, Manchester City kwa pointi nane baada ya michezo 11 tu.

Kipigo cha Jumapili kutoka kwa Chelsea, ni mechi ya tatu mfululizo ya ugenini Mourinho kutoka bila ushindi, hii ni baada ya kufungwa na Huddersfield na kuokota sare kwa Liverpool.

Ince anasema timu hiyo inakosa kiongozi, jambo lililowagharimu kwenye mchezo dhidi ya Chelea.

Akiongoea na Dail Maily la Uingereza, Ince alisema: “Nilitazama kupitia televisheni Huddersfield ikiichapa Manchester United mwezi uliopita na wakati nikifurahishwa na mwanangu Thomas, nikagundua kuwa kuna upungufu wa wachezaji viongozi kwa United.
  
"Enzi zetu wachezaji viranja tulikuwa wengi, niliweza kumpigia kelele Roy Keane, yeye pia alinipigia kelele za kuniweka sawa, Gary Pallister hali kadhalika. 

"Phil Jones anajaribu kidogo kufanya hivyo, nadhani ndiyo maana Mourinho anampenda, lakini alipoumia na kutoka hakuna mwingine aliyebeba jukumu lake.”
No comments