PICHA 10: MSONDO NGOMA ILIVYOMIMINA RHUMBA HUKU MVUA IKIKUNG’UTA DAR SAFARI PARK

JUMAMOSI ilikuwa ni siku ambayo mvua kubwa ilipiga kutwa kucha, hususan jijini Dar es Salaam ambapo kwa upande shughuli za muziki, bendi nyingi zililazimika kuvunja shoo zake.

Lakini hali hiyo ilikuwa ni tofauti kwa upande wa Msondo Ngoma wanaotumbuiza ndani ya dar Safari Park kila wiki katika siku kama hiyo, ambapo pamoja na mvua kuunguruma ipasavyo, bado rhumba lilirindima na mashabiki kuonekana kuchizika  vilivyo.


“Naomba Ushauri Wenu”, “Kiapo”, "Binti Maringo", “Mama Kossy”, “Pricillar” na “Kilio cha Mtu Mzima” ni kati ya vigongo vilivyorindimishwa na kuwanyanyua mashabiki vitini ambao wengine walionekana hadi kujitosa mvuani kwa raha za kuusakata Msondo.
 Abdul Ridhiwan "Pangamawe" akiwa kazini
 Mcharazaji bess gitaa akinogesha uhondo
 Mwimbaji Juma katundu akiimba kwa hisia kali
 Hapa Hassan Moshi akiwacharusha mashabiki kwa sauti yake tamu ya urithi
 Roman Mng'ande "Romarii" akipuliza tarumbeta na kuongeza msisimko wa muziki
 Mcharazaji chips Saad Ally "Machine" akiongoza uhondo
 Mwimbaji Eddo Sanga akinung'unika mbele ya mashabiki wao
 Said Mabera akifanya yake
 Twaha Malovee nae hakuwa nyuma katika kuwabembeleza mashabiki kwa sauti yake murua
Athuman Kambi akiwajibika kiume

No comments