PICHA 22: MAZISHI YA “PALI PALI” MDOGO WAKE NYOSHI EL SAADAT YALIVYOFANYIKA SINZA


Jumanne iliyopita iliyopita ilikuwa ndiyo siku aliyopumzishwa kwenye makazi yake ya milele Morrice Kisaba Matala (Pali Pali) ambaye ni mdogo wake na mwanamuziki nyota wa dansi Nyoshi el Saadat.

Pali Pali ambaye alifariki Jumamosi ya Novemba 18 baada ya kuugua kwa muda mrefu, alizikwa katika makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam.

Mazishi ya Pali Pali aliyekuwa mtu wa watu, yalidhuhuriwa na kiasi kikubwa cha wadau wa muziki pamoja na wanamuziki wengi wakiwemo wa bendi za FM Academia, Twanga Pepeta, Malaika Band, Mapacha Music Band na nyingine nyingi.
 Wanamuziki Totoo ze Bingwa (kushoto) na Ibonga Katumbi Jesus wakiwa msibani muda mfupi kabla ya kuelekea makaburini
 Waombolezaji wakipata chakula nyumbani kwa Nyoshi, Sinza jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea makaburi ya Sinza
 Wadau na wanamuziki wakiwa nyumbani kwa Nyoshi kwenye msiba wa Pali Pali
 Kaposhoo Tumba (kushoto) akiwa na Rama Pentagon
 Mandhari ya msiba wa Pali Pali
 Sanduku lililobeba mwili wa Pali Pali
 Nyoshi akiwa na mwanae wa kwanza, Stalone
 Baadhi ya wanamuziki waliohudhuria mazishi ya Pali Pali. Kutoka kushoto ni King Blaise, Patcho Mwamba, Kardinal Gento na Papaa Noah
 Safari ya kuelekea makaburini inaanza
Gari lililobeba mwili wa Pali Pali
 Mwili wa Pali Pali unawasili makaburi ya Sinza
 Sehemu ya watu waliohudhuria mazishi ya Pali Pali
 Sanduku lenye mwili wa Pali Pali likiingizwa kaburini
 Wadau na wanamuziki
 Nyota wa bongo fleva Dully Sykes akimpa pole Nyoshi makaburini
 Mbunge wa Korogwe vijijini Profesa Maji Marefu (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na wanamuziki makaburi ya Sinza wakati wa kumzika Pali Pali
 Profesa Maji Marefu na wanamuziki
 Nyoshi akimfariji binti yake
 Kiongozi wa Twanga Pepeta Luizer Mbutu naye alikuwepo makaburini
 Dj Bullah wa Clouds FM (kushoto) alikuwa sehemu ya watu waliomzika Pali Pali
 Wanamuziki mbali mbali walihudhuria mazishi ya Pali Pali
Nyoshi akiwa na familia yake pamoja na rafiki zake

No comments