PICHA 7: ISHA MASHAUZI NA CHRISTIAN BELLA WASANII PEKEE WA TAARAB NA DANSI WALIOTUMBUIZA KILELE CHA FIESTA 2017


Hatimaye msimu wa Fiesta 2017 ulifikia tamati Jumamosi usiku kwa tamasha kubwa la kukata na shoka lililofanyika Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Tamasha hili kubwa kuliko matamasha yote ya burudani, likapambwa na wasanii nyota wa muziki wa kizazi, huku kila mmoja akijaribu kulinda  heshima ya jina lake jukwaani.

Christian Bella akawa mwimbaji pekee wa muziki wa dansi aliyepewa heshima ya kutumbuiza kwenye fainali hiyo ya Fiesta huku mwimbaji bora wa kike wa taarab, Isha Mashauzi akiwa msanii pekee wa taarab kutumbuiza katika onyesho hilo la Fiesta.

Hakuna shaka kuwa uwezo wa Bella na Isha wa kujibadilisha kama kinyonga na kwenda sambamba na mahitaji ya soko la muziki, ndiyo sababu kubwa ya kuchaguliwa kwao kwenye tamasha la Fiesta ambalo limeegemea zaidi katika muziki wa kizazi kipya.
 Christian Bella akikamua kwenye jukwaa la Fiesta
 Bella akiwa sambamba na Ommy Dimpoz
 Isha Mashauzi akijinafasi kwenye jukwaa la Fiesta
 Isha Mashauzi jukwaani
 Isha akienda sambamba na Barnada katika wimbo "Nimpe Nani"
Isha Mashauzi msanii pekee wa taarab kutumbuiza kwenye kilele cha Fiesta
Christian Bella mwimbaji pekee wa dansi kutumbuiza katika kilele cha Fiesta


No comments