RAHMA MACHUPA AIAMBIA SALUTI5: NI ‘KWELI NIMEREJEA JAHAZI’ …asema mambo ya mkataba atayajua mbele kwa mbele


Mwimbaji staa wa wimbo “Nipe Stara”, Rahma Machupa, amefunguka kuwa ni kweli amerejea Jahazi Modern Taarab.

Jana usiku Rahma Machupa alitambulishwa na Jahazi Modern Taarab ndani ya ukumbi wa Dar Live.

Hata hivyo Rahma Machupa hiyo jana hakuongea lolote juu ya safari yake ya kurejea Jahazi na badala yake kila neno lilizungumzwa na kiongozi wa bendi Prince Amigo.

Saluti5 jioni hii imemtafuta Rahma Machupa kwa njia ya simu ili kuthibitisha kama ni kweli amerejea Jahazi au ilikuwa ni gumzo la kufurahisha baraza tu kutoka kwenye kinywa cha Amigo.

Rahma bila kupepesa macho akaithibitishia Saluti5 kuwa ni kweli ameamua kurejea Jahazi Modern Taarab.

“Ni kweli nimeamua kurejea Jahazi, nimerudi nyumbani kwahiyo kuanzia sasa mimi ni msanii wa Jahazi Modern Taarab,” alisema Rahma Machupa.

Saluti5 ilipoumiliza Rahma juu ya mkataba wake na Wakali Wao Modern Taarab ambao unaaminika bado haujaisha, mwimbaji huyo akasema hayo yatajulikana baadae.

“Mambo ya hatma ya mkataba yatajulikana baadae, watakachoamua wao Wakali Wao na mimi ndiyo nitajua hatua ya kuchukua kuhusu hicho kinachoitwa mkataba”, alihitimisha Rahma.

No comments