RAMA PENTAGONE ATOA SOMO LA UVUMILIVU KWA WANAMUZIKI WA DANSI... asema "jamani tusiendekeze njaa"

MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Dansi, Rama Pentagone ametoa ushauri wa bure kwa wasanii wenzake wa miondoko hiyo kwa kuwaambia wanapaswa kuwa wavumilivu kwenye bendi zao, hasa kwa upande wa maslahi, iwapo wanahitaji heshima ya kweli kimuziki.

Pentagone ambaye ni kati ya waimbaji na watunzi wenye uwezo mkubwa, aliyewahi kutamba vilivyo na makundi kadhaa ya dansi yakiwemo Extra Bongo, Twanga Pepeta na Ivory Band, amesema: “Haiwezi kuwa rahisi kwako kuilinda heshima ikiwa utaendekeza njaa.”

Amesema anayo mifano ya wanamuziki wengi ambao wamejikuta wakishuka thamani kutokana na kukosa uvumilivu hasa pale wanapopita katika mapito magumu ya kikazi.


“Uvumilivu ndio ngao ya kwanza katika sekta yoyote ile, hata katika mapenzi. Kama huna uvumilivu huwezi kudumu hata katika ndoa ama mahusiano yako na mpenzio kwani muda wote utakuwa anaangalia wengine waliomzidi huyo uliyenae kwa wakati huo,” amesema Pentagone.

No comments