RAPA WA KINIGERIA AKATAA KUSHINDANISHWA NA DAVIDO, VIZKID... asema yeye ni "bwamdogo" sana

RAPA Bolaji Ojudokan ambaye anajulikana kwa jina la Boj amesema kuwa hafanyi muziki ili kushindana na mastaa Davido na Wizkid.

Rapa huyo amesema kuwa anafanya muziki kama starehe na wala hana lengo la kushindana na mastaa wakubwa kama ambavyo jamii imekuwa ikimtafsiri.

“Muziki ni sehemu ya maisha yangu, ni kitu ambacho nilikipenda tangu nikiwa na umri mdogo hivyo sipo hapa kwa ajili ya mashindano ila nafurahi kufikia ndoto zangu,” alisema staa huyo.


“Sikuwahi kudhani naweza kufika hapa nilipo maana utotoni kilikuwa kitu cha kujifurahisha tu hivyo kunilinganisha na Davido na Wizkid sio sawa.” 

No comments