RASHID PEMBE ACHEKELEA WANAFUNZI KUPAPATIKIA DARASA LAKE LA BURE LA SAXAPHONE

MKONGWE wa Saxaphone, Rashid Pembe amesema kuwa anafarijika kuona anazidi kupokea wanafunzi katika darasa lake la bure la kujifunza upulizaji wa chombo hicho cha muziki.

Hivi karibuni mkongwe huyo alitoa ofa ya kuwafundisha bure vijana watakaokuwa tayari kuchukua ujuzi wa saxophone, ikiwa ni awamu ya pili kufanya hivyo ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka juzi alipofanikiwa kuwaibua vijana takriban 17.


Darasa hilo la Domo la Bata linaendelea nyumbani kwake Mwananyamala, jijini Dar es Salaam na tayari wanafunzi zaidi ya 10 wameshajitokeza huku wengine wakiahidi kuzidi kumiminika. 

No comments