RASHID PEMBE AJA NA OFA YA KUFUNDISHA BURE SAXAPHONE

MPULIZAJI Saxaphone nguli, Rashid Pembe ametoa ofa ya kufundisha bure chombo hicho kwa wanaohitaji, ambapo tayari watu wameanza kujitokeza kuchukua kozi nyumbani kwake, Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.

“Nafurahi kuona watu wanamiminika ambapo hivi sasa ndio kwanza mwezi wa pili tangu nitoe ofa hii na tayari nina vijana watano huku wengine zaidi wakiahidi kuja kupata ujuzi huu,” amesema Pembe anayejulikana pia kwa jina la “Professor”.

 Hii ni mara ya pili kwa Pembe kuja na ofa kama hii ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni miaka mitatu nyuma walipojitokeza vijana 17 aliowafundisha na kufaulu vyema ambapo sasa wamepata ajira sehemu tofauti tofauti.


Pembe amesema kuwa ingawaje hana kipato chochote anachoingiza kutokana na ofa hiyo lakini binafsi anafarijika kuona anaingia kwenye orodha ya wanamuziki wanaochangia kuongeza idadi ya watumiaji ala hiyo hapa nchini. 

No comments