RASHID SUMUNI ACHAFUA HALI YA HEWA SAKATA LA KUTIWA MATATANI KING KIKII

MCHARAZAJI mahiri wa gitaa kiongozi la Solo hapa nchini, Rashid Sumuni ameonekana kuikumbusha kuwa jamii sheria ni msumeno na kwamba kisichofaa huyu basi hata kwa mwingine pia kisiachwe ama kushangiliwa.

Katika posti yake aliyoitoa kwenye ukurasa wake wa facebook, nguli huyo ameonekana kushangazwa na kitendo cha wadau wengi kulalamikia sheria ya kumaliza muziki saa 6:00 usiku, baada tu ya hivi karibuni kutiwa matatani kwa mkongwe King Kikii.


“Dah!! Wahenga tumelalamika weee kuh sheria ya kumaliza saa 6 Wala hatukueleweka kabisa, sasa yanawakuta kina flani we!!!!!! Inaonekana watu sasa ndio wamebanwa!!? Ama kweli yatima hadeki....” ameandika Sumuni katika posti hiyo.

No comments