RASHID SUMUNI AFICHUA KILICHOJIFICHA KATI YAKE NA RAMA PENTAGONE

RASHID Sumuni aliyeungana na nguli mwenzie, Rama Pentagone katika bendi mpya ambayo hivi sasa iko katika mchakato wa kukamilisha usajili, amesema anaamini watafika mbali wakiwa na bendi hiyo, hasa kutokana na kukusanya kundi dogo la wanamuziki lakini wanaojielewa.

Akiongea na Saluti5 jioni hii, Sumuni amesema kuwa, pamoja na mambo mengine yote, kikwazo kikubwa kinachosababisha bendi nyingi kutoyafikia malengo wanayojiwekea, ni bendi hizo kuwa na lundo la wanamuziki wasio na malengo.

“Niko na swahiba wangu Rama (Pentagone), tumeamua kufanya kitu fulani ambacho tunajua kitaanza kwa wengine kukibeza lakini mwisho wa siku, kutokana na msimamo tulionao, tulichokusudia kitaonekana na wote watafunga midomo,” amesema Sumuni.

Sumini amewataja baadhi ya wasanii walionao ndani ya bendi hiyo kuwa ni pamoja na waimbaji; Joyce, mzee Abraham na wapiga ala Peter (drums), Awadh (kinanda) na Athuman kwenye gitaa la besi.

No comments