REAL MADRID CHA MTOTO KWA TOTTENHAM, YACHAPWA 3-1 … Borussia Dortmund 1 - 1 Nicosia


Real Madrid kwa Tottenham imekuwa  nyanya zaidi ya ujuavyo baada ya kukubali kichapo cha bao 3-1 kwenye mchezo wa kundi H wa Ligi ya Mabingwa.

Hadi dakika ya 79, Tottenham ilikuwa mbele 3-0 kwa mabao ya Dele Alli aliyefunga mara mbili dakika ya 27 na 56 huku lingine likifungwa na Christian Eriksen dakika ya 65.

Cristiano Ronaldo akaipatia Real Madrid bao la kufutia machozi dakika ya 80.

Zikiwa zimesalia mechi mbili, Tottenham iko kileleni kwa pointi 10 huku Real Madrid ikishika nafasi ya pili kwa pointi 7.

Katika mchezo mwingine wa kundi H timu za Borussia Dortmund na Nicosia zilitoshana nguvu kwa sare ya 1-1.

No comments