REAL MADRID YAACHANA NA DE GEA, SASA YAMALIZANA NA KIPA ARRIZABALAGA WA ATHLETIC BILBAO


Real Madrid itaachana na mpango wa kumwania kipa wa Manchester United David de Gea baada ya kufikia makubaliano ya kumyakua kipa Kepa Arrizabalaga wa Athletic Bilbao.
Mabingwa hao wa Champions League wamekuwa sokoni kusaka kipa mpya wa kuchukua nafasi ya Keylor Navas.
Kwa mujibu wa mwandishi Pipi Estrada wa Hispania, Real Madrid tayari imefikia makubaliano na Athletic Bilbao juu ya kupata saini ya Kepa.


No comments