REAL MADRID YAANZISHA HARAKATI ZA KUMSAJILI NEYMAR ILI AKARITHI MIKOBA YA RONALDO


Imeripotiwa kuwa rais wa Real Madrid amekutana na baba mzazi wa Neymar kwaajili kujadili mpango wa kumrejesha Hispania mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona ili akazibe nafasi ya Cristiano Ronaldo.

Neymar ndiyo kwanza ametua PSG kiangazi kilichopita akitokea Barcelona kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia - pauni milioni 198.

Tangu ametua PSG, Neymar amefunga mara 11 katika mechi 12 alizocheza.

Real Madrid walitaka kumsaji Neymar kutokea Santos ya Brazil mwaka 2013 lakini badala yake akachagua Barcelona ambako alifanikiwa kushinda taji moja la Champions League katika miaka minne aliyoitumikia klabu hiyo.

Lakini milango ya kutua Bernabeu bado iko wazi kwa Neymar — ingawa hilo litatimia pale tu Ronaldo atakapomaliza mkataba wake mwaka 2021.

No comments