REAL MADRID YATENGA PAUNI MIL 80 KUMSAJILI ANTHONY MARTIAL


Real Madrid itajaribu kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial kwa kuweka mezani pauni milioni 80.

Wakati safu ya ushambuliaji ya Real Madrid inayoongozwa na Cristiano Ronaldo na Karim Benzema ikionekana butu msimu huu, kocha Zinedine Zidane atajaribu kumnunua Martial kiangazi kijacho.

Martial amekuwa kwenye 'fomu' nzuri msimu huu na tayari ameishaifungia Manchester United mabao matano ya Premier League.
No comments